When a young Eva Kollisch arrives as a refugee in New York in 1940, she finds a community among socialists who share her values and idealism. She soon discovers ‘the cause’ isn’t as idyllic as it seems. Little does she know this is the beginning of a lifelong commitment to activism and her determination to create radical change in ways that include belonging, love and one's full self. In addition to Eva Kollisch’s memoirs Girl in Movement (2000) and The Ground Under My Feet (2014), LBI’s collections include an oral history interview with Eva conducted in 2014 and the papers of Eva’s mother, poet Margarete Kolllisch, which document Eva’s childhood experience on the Kindertransport. Learn more at www.lbi.org/kollisch . Exile is a production of the Leo Baeck Institute , New York | Berlin and Antica Productions . It’s narrated by Mandy Patinkin. Executive Producers include Katrina Onstad, Stuart Coxe, and Bernie Blum. Senior Producer is Debbie Pacheco. Associate Producers are Hailey Choi and Emily Morantz. Research and translation by Isabella Kempf. Sound design and audio mix by Philip Wilson, with help from Cameron McIver. Theme music by Oliver Wickham. Voice acting by Natalia Bushnik. Special thanks to the Kollisch family for the use of Eva’s two memoirs, “Girl in Movement” and “The Ground Under My Feet”, the Sophia Smith Collection at Smith College and their “Voices of Feminism Oral History Project”, and Soundtrack New York.…
Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu
Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu
Kutana na Francine Aka Epse Akaanghui Rais wa Chama cha wanasheria wanawake nchini Côte d'Ivoire huko Afrika Magharibi. Yeye anashiriki mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 akisema taifa lake lina mengi ya kujivunia wakati huu wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji. Francine amezungumza na Assumpta Massoi katika makala hii.…
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox’s Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini kwanza ni makala ambapo Assumpta Massoi anazungumza na mshiriki wa CSW69 kutoka Cote D’Ivoire.Na katika mashinani Felicite Djoukouo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Maendeleo nchini Cameroon ambaye anashiriki mkutano wa CSW69 hapa Umoja wa Mataifa anaelezea matarajio yake ya mkutano huu utakaomalizika tarehe 21 mwezi huu wa Machi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!…
Leo Ijumaa ikiwa ni siku ya 11 ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefuturu na wakimbizi wa Rohingya walioko kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox Baazar nchini Bangladesh kuonesha mshikamano na wakimbizi na wenyeji wanaowahifadhi. Anold Kayanda na maelezo zaidi.…
Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.…
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua neno Wakfu.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii imezungumza na Lucy Gidamis, Wakili ambaye kwa sasa anafanya kazi na shirika la Msichana Initiative nchini Tanzania akijikita katika kutetea na kutekeleza haki za wanawake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno Wakfu.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya duniani WHO na la kuhudumia watoto UNICEF yametangaza kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa surua barani ulaya, jumla ya wagonjwa 127,350 waliripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40.Na hii leo ikiwa ni chungu cha 10 cha Ramadhan, ikikamilisha fungu la kwanza kati ya mafungu matatu ambapo ni siku 30 za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameanza ziara yake ya siku nne nchini Bangladesh ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka wa kushiriki Ramadhan na jamii za waislamu walio kwenye changamoto mbalimbali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua neno Wakfu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!…
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.…
Hii leo jaridani tunaangazia mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80, na yaliyojiri katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa..Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.Makala tukisalia hapa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani ambako Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu, nimezungumza na Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.Na Katika mashinani fursa ni yake Janet Zebedayo Mbene kutoka Tanzania aliyehududhuria mkutano huu hapa makao makuu, kama mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa uwezeshaji wa wanawake Tanzania na angependa kuwashauri wanawake na wasichana wanaopitia changamoto wajikite katika fursa mbalimbali. Kila kitu kina changamoto. Wajitie moyo na waondoe uoga, na kwa kile kidogo walicho nacho wanaweza kujiinua na kuinua jamii kwa ujumla.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!…
Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.…
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa kina inayomulika mkutano wa CSW69 ulioanza Jana Jumatatu hapa New York, Marekani, ikiwa ni miaka 30 tangu mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995, ukiweka msingi wa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ya usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari na sauti za vijana kutoka mashinani.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekutana na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wanaoshiriki Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69. Bwana Guterres amezitaka Asasi za Kiraia kuendelea kuzisukuma nchi kuweka mazingira bora kwa ajili ya usawa wa wanawake na wasichana na pia akakumbushia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwaunga mkono katika kulitimiza lengo hilo.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk kupitia Msemaji wake, ameripoti ukatili unaoendelea katika pwani ya Syria tangu Machi 6, ambapo anasema takriban raia 111 wameuawa, wengi wao kwa misingi ya kiimani. Hospitali pia zimeshambuliwa na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa uchunguzi huru na uwajibikaji kwa wahusika.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Malawi limeongeza wigo wa mpango wake wa Mlo Shuleni unaopatikana kwa kununua vyakula vinavyolimwa na wananchi wa karibu katika maeneo hayo. Mradi huo unaotekelezwa wilayani Nkhotakota, unanufaisha wanafunzi 10,000 na kusaidia wakulima wadogo 1,200, hivyo kuimarisha upatikanaji wa chakula na uchumi wa ndani.Na Katika mashinani huku mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukiendelea hapa makao makuu, tutakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe wa vijana kuhusu usawa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!…
Fatuma Mfumia ndiye dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania. Fatuma ndiye tunayemwangazia leo. Video iliyorekodiwa na UNICEF Tanzania inamwonesha akiwa kwenye usukani, na hakika hapo utakubali anavyojiamini. Anold Kayanda na simulizi zaidi.
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000. Selina Jeroboni na taarifa zaidi.…
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 na wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC kwenda Burundi. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon, kulikoni?Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000.Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi.Makala leo tunamwangazia Fatuma Mfumia, dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhuduia Watoto, UNICEF Tanzania.Na mashinani mashinani fursa ni yake Ghada Dawiche’s ambaye licha ya machungu yaliyomkumba baada ya kupoteza bintiye aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Lebanon, pamoja na mjukuu wake wa kiume wakati kombora la Israeli lilipopiga nyumba yao nchini Lebanon, anasema Umoja, nguvu na tumaini ndio ujumbe mkuu anaowapa wanawake wote waliopoteza wapendwa wao vitani na katika kupigania haki za wanawake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!…
Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.…
Player FM'e Hoş Geldiniz!
Player FM şu anda sizin için internetteki yüksek kalitedeki podcast'leri arıyor. En iyi podcast uygulaması ve Android, iPhone ve internet üzerinde çalışıyor. Aboneliklerinizi cihazlar arasında eş zamanlamak için üye olun.
En sevdiğin şovları internet üzerinden yönetmek ve Adroid ve iOS uygulamalarımızda çevirim dışı dinlemek için dünyanın en iyi podcast uygulamasına katılın. Ücretsiz ve kolay!