14 MACHI 2025
Manage episode 471424102 series 2027789
İçerik UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations tarafından sağlanmıştır. Bölümler, grafikler ve podcast açıklamaları dahil tüm podcast içeriği doğrudan UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations veya podcast platform ortağı tarafından yüklenir ve sağlanır. Birinin telif hakkıyla korunan çalışmanızı izniniz olmadan kullandığını düşünüyorsanız burada https://tr.player.fm/legal özetlenen süreci takip edebilirsiniz.
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox’s Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini kwanza ni makala ambapo Assumpta Massoi anazungumza na mshiriki wa CSW69 kutoka Cote D’Ivoire.Na katika mashinani Felicite Djoukouo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Maendeleo nchini Cameroon ambaye anashiriki mkutano wa CSW69 hapa Umoja wa Mataifa anaelezea matarajio yake ya mkutano huu utakaomalizika tarehe 21 mwezi huu wa Machi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
…
continue reading
100 bölüm