Kenya : Haki ya raia kuandamana kufikisha ujumbe kwa serikali
Manage episode 425534307 series 1220196
Nchini Kenya vijana wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Idadi kubwa ya vijana hao wanapinga mswaada huo wanaosema utaongeza gharama ya maisha kipindi hiki wengi wao wakiwa tayari hawana ajira, makali ya gharama ya maisha nayo yakiendelea kulemaza shughuli zao za kila siku.
Maandamano hayo yameandliwa na kundi la vijana linalojiita Gen Z, yaani kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya mwaka 1995 hadi 2010.
Vijana hawa wanadai serikali ya rais William ruto imeanza kuwa dhalimu kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa muhimu kama vile soda za wanawake na vinengnevyo.
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
24 bölüm